Leo katika mkutano wa hadhara kata ya Levolosi, Jimbo la Arusha Mjini. Hakika wananchi wanazidi kuhamasika.
Tukutane kesho kwenye maandamano ya amani.
#VuguvuguLaKudaiHaki
Nikiwa mtaa kwa mtaa katika jiji la Arusha. Kuhakikisha wananchi wanapata taarifa ya maandamano tarehe 27 Februari 2024.
#VuguvuguLaKudaiHaki
Naelezwa, baada ya ufuatiliaji wa kutosha, tumebaini huyu ndiye mtu anayepiga picha za pembeni na katika vilinge ambavyo maandamano hayajafika kuonesha kwamba maandamano hayana watu. Tunaweza kushughulika naye au tumpotezee tu? #vuguvugulakudaihaki
Viwanja vya Ruanda-Nzovye,Mbeya, mvua imenyesha kubwa sana, tumelazimika kuhairisha mkutano wetu hapa, tutarudi tena Mbeya. Licha ya mvua kunyesha kubwa, lakini wananchi wa Mbeya wamejitokeza wa kutosha sana. Tunawashukuru sana. ππΎππ½ #PeoplesPower #vuguvugulakudaihaki
Maandamano Tanga yakiwa yamefika eneo la Tangamano.
#WikiYaMaandamano
#VuguvuguLaKudaiHaki
MAANDAMANO YA AMANI MBEYA
Njia ya Uyole Mhe.Joseph Mbilinyi(Sugu) Mstari wa Mbele.
#Vuguvugulakudaihaki
MAANDAMANO YA AMANI MBEYA
Kituo Cha uyole Jijini Mbeya anaongoza Makam Mwenyekiti CHADEMA Taifa Mhe.Tundu Lissu Burudani inaendelea.
#Vuguvugulakudaihaki .
Maandamano yakiwa yamefika maeneo ya Usalama, yakielekea Shekilango, ambapo yataungana na maandamano yaliyoanzia Mbezi mwisho.
#VuguvuguLaKudaiHaki
NJIA YA MAKAM MWENYEKITI TUNDU LISSU - viwanja vya furahishwa ikiongozwa na katibu.
#vuguvugulakudaihaki
Bariadi Simiyu wananchi wamejitokeza kwa wingi kuunga mkono
Maandamano yameongozwa na Mh Freeman Mbowe
Mwenyenzi CHADEMA Taifa #WikiYaMaandamano .
#VuguvuguLaKudaiHaki
Arusha tayari kwa maandamano makubwa ya kihistoria Tarehe 27/02/2024, Kila mmoja wetu anajukumu hilo kubwa la kuhakikisha sauti zinaunganishwa na kupazwa kwa pamoja,Mtawala anayejielewa husikiliza sauti za Wananchi na mtawala asiyejielewa hupuuza Wananchi.
#VuguvuguLaKudaiHaki
Soko la Samunge, Arusha. Mvua kubwa imepiga lakini mkasema βhapanaβ tutaandamana tu. Mmetupa heshima kubwa sana Arusha. #vuguvugulakudaihaki #peoplespower
Maandamano Tanga yakiwa yamefika eneo la Tangamano.Tanga imeiva !
#WikiYaMaandamano
#VuguvuguLaKudaiHaki
Kamanda DEUSDEDITH SOKA akihamasisha wananchi Kushiriki kwenye Maandamano jijini Arusha huku akibainisha umuhimu wa kuwa na #KaribaMpya kwa ustawi wa nchi.
#VuguvuguLaKudaiHaki